Mkuu wa Kitengo cha JEMA AUTO ameeleza sababu kuu zinazofanya Watanzania waichague JEMA AUTO kama mshirika wao bora wa kuagiza magari kutoka Japan.
Amefafanua kuwa JEMA AUTO inatoa bei nafuu na shindani kwa sababu kampuni hununua magari moja kwa moja kwenye minada ya Japan bila kupitia mawakala wa kati. Wakala wengi nchini hutegemea mawakala walioko Japan, hali inayopelekea kuongezeka kwa gharama za ununuzi kwa wateja.
Kupitia mfumo wetu wa Live Bidding, mteja anashiriki moja kwa moja katika kuchagua na kununua gari lake kwa uwazi na bila gharama zisizo za lazima. Huu ndio msingi unaoifanya JEMA AUTO kuwa chaguo sahihi, salama na rafiki kwa kila Mtanzania anayehitaji gari bora kwa bei halisi ya mnadani.
“Mfumo huu umeondoa kikwazo cha safari ndefu na gharama kubwa za kwenda Japan. Sasa mteja anaweza kununua gari popote alipo, akitumia simu au kompyuta, ndani ya muda mfupi na kwa uaminifu,” alisema mmoja wa wawakilishi wa kampuni.
Kampuni ya uuzaji wa magari kutoka Japan, JEMA AUTO, kupitia akaunti yao ya @jema_auto_tz, imezindua mfumo wa kisasa wa mnada wa magari mtandaoni unaowawezesha wanunuzi kushiriki moja kwa moja kupitia tovuti maalumu—bila kulazimika kusafiri nje ya nchi.
Kupitia mfumo huo, wateja na mawakala wanaweza kufikia zaidi ya magari 400,000 kwa siku, yote yakipatikana kwa njia ya ushindani wa wazi mtandaoni. Hatua hii imeelezwa kama mapinduzi makubwa katika sekta ya uagizaji wa magari kutoka nje, hususan kutoka Japan.
Kwa mujibu wa waandaaji wa mfumo huo, lengo kuu ni kufanya upatikanaji wa magari uwe rahisi, salama na nafuu, huku mteja akinunua kwa uwazi na bila wasiwasi kuhusu gharama za ziada.

Faida Kuu za Mfumo wa Live Bidding
Miongoni mwa faida zinazotolewa na mfumo huu ni pamoja na:
- Uwazi wa taarifa na mchakato mzima wa mnada
- Urahisi wa kufuatilia mwenendo wa mnada kwa wakati halisi
- Kupata magari bora kwa bei nafuu kutokana na ushindani wa moja kwa moja
-
Usalama na faragha—mteja hushiriki bila taarifa zake kuonekana kwa watu wengine
Mfumo huu umeundwa kuhakikisha mteja anapata thamani halisi ya pesa yake bila usumbufu.
Kampeni Maalumu ya Mwisho wa Mwaka
JEMA AUTO pia imetangaza kampeni maalumu ya mwisho wa mwaka yenye zawadi mbalimbali kwa wateja.
Kila mteja atakayenunua gari kupitia mfumo huu atapata zawadi ya TZS 200,000.
Zaidi ya hapo, kutakuwa na zawadi nyingine za thamani kama kompyuta mpakato (laptops) na vifaa vingine kwa washindi watakaopatikana.
Kampeni hii itakamilika tarehe 31 Desemba 2025, na inalenga kuhamasisha matumizi ya teknolojia katika ununuzi wa magari kwa njia salama, nafuu na ya uwazi.
Kwa sasa, mfumo huu unapatikana mtandaoni na tayari umevutia mamia ya wanunuzi wapya nchini wanaotafuta magari ya binafsi na ya biashara bila usumbufu kutoka nje ya nchi.
